TAARIFA KWA UMMA

UTEUZI NA UHAMISHO WA VIONGOZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi kwa kuwateua Waziri na Naibu Waziri, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu; kuwahamisha wizara baadhi ya Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu pamoja na kumteua Mkurugenzi wa Uchaguzi. Aidha, Mheshimiwa Rais amefanya uhamisho wa Mkuu wa Mkoa mmoja. Katika mabadiliko hayo, Mheshimwa Rais pia amehamishia majukumu ya Uwekezaji katika Ofisi ya Rais. Vilevile, amefuta nafasi ya Katibu Mkuu (Uvuvi) na badala yake Wizara ya Mifugo na Uvuvi itakuwa na Katibu Mkuu mmoja na Naibu Makatibu Wakuu wawili. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:

A: Uteuzi wa Waziri na Naibu Waziri

Mheshimiwa Rais amewateua wafuatao:

  1. Mhe. Abdallah Hamis Ulega kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Mhe. Ulega anachukua nafasi ya Mhe. Mashimba Ndaki ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
  1. Mhe. Hamis Mohamed Mwinjuma kuwaNaibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Mwinjuma anachukua nafasi ya Mhe. Pauline Philipo Gekul ambaye amehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria.

B: Uhamisho wa Naibu Mawaziri

Mheshimiwa Rais amewahamisha wizara Naibu Mawaziri wafuatao:

  1. Mhe. Pauline Philipo Gekul amehamishwa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.
  1. Mhe. Geofrey Mizengo Pinda amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwenda kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
  1. Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete amehamishwa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenda kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
  1. Mhe. Deogratius John Ndejembi amehamishwa kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwenda kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI.
  1. Mhe. David Ernest Silinde amehamishwa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kwenda kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

C: Uteuzi na Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa

Mheshimiwa Rais amewateua Wakuu wa Mikoa wafuatao:

  1. Bibi Christina Solomon Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Bibi Mndeme anachukua nafasi ya Bibi Sophia Edward Mjema ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi – Itikadi na Uenezi.
  1. Dkt. Francis Kasabubu Michael kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Kabla ya uteuzi Dkt. Michael alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
  1. Aidha, Mheshimiwa Rais amemhamisha Mhe. Wazir Kindamba kutoka Mkoa wa Songwe kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga kuchua nafasi ya Bw. Omary Tebweta Mgumba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

D: Uteuzi na Uhamisho wa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu

Mheshimiwa Rais amewateua Makatibu Wakuu wapya wafuatao:

  1. Dkt. Tausi Mbaga Kida – Ofisi ya Rais (Uwekezaji)
  • Bw. Juma Selemani Mkomi – Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Balozi Samwel William Shelukindo – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  • Prof. Carolyne Ignatius Nombo – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
  • Bw. Gerald Geofrey Mweli – Wizara ya Kilimo
  • Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe – Wizara ya Afya
  • Mhandisi Nadhifa Sadiki Kemikimba – Wizara ya Maji
  • Bw. Kheri Abdul Mahimbali – Wizara ya Madini
  • Bw. Mohamed Abdulla Khamis – Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Aidha, Mheshimiwa Rais amewabadilisha wizara Makatibu Wakuu wafuatao:

  1. Prof. Riziki Sailas Shemdoe kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda Wizara ya Mifugo na Uvuvi
  • Dkt. John Anthony Jingu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) kwenda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
  • Dkt. Jim James Yonazi kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
  • Bw. Adolf Hyasinth Ndunguru kutoka Wizara ya Madini kwenda Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
  • Mhandisi Anthony Damian Sanga kutoka Wizara ya Maji kwenda Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Vilevile Mheshimiwa Rais amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya wafuatao:

  1. Dkt. Wilson Mahera Charles – Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya). Kabla ya uteuzi, Dkt. Charles alikuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
  • Bw. Sospeter Mambile Mtwale Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Kabla ya uteuzi, Bw. Mtwale alikuwa Afisa Mwandamizi Ofisi ya Rais Ikulu.
  • Dkt. Franklin Jasson Rwezimula – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia(Elimu ya Msingi na Sekondari). Kabla ya uteuzi, Dkt. Rwezimula alikuwa Meneja wa NEMC Kanda ya Kati.
  • Dkt. Hussein Mohamed Omar – Wizara ya Kilimo. Kabla ya uteuzi, Dkt. Omar alikuwa Afisa Mwandamizi Ofisi ya Makamu wa Rais.
  • Bw. Cyprian John Luhemeja – Wizara ya Maji. Kabla ya uteuzi, Bw. Luhemeja alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA.
  • Bi. Lucy Dominico Kabyemera – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi, Bi Kabyemera alikuwa Mkurugenzi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
  • Bw. Anderson Gukwi Mutatembwa – Wizara ya Maliasili na Utalii. Kabla ya uteuzi, Bw. Mutatembwa alikuwa Afisa Mwandamizi Ofisi ya Rais Ikulu.
  • Bw. Athuman Selemani Mbuttuka – Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi, Bw. Mbuttuka alikuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani.
  • Dkt. Daniel Elius Mushi – Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo). Kabla ya uteuzi, Dkt. Mushi alikuwa Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania.
  1. Bibi Agnes Kisaka Meena – Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi). Kabla ya uteuzi, Bibi Meena alikuwa Mkurugenzi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
  1. Bw. Selestine Gervas Kakele – Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kabla ya uteuzi, Bw. Kakele alikuwa Afisa Mwandamizi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Rais pia amewahamisha wizara Naibu Makatibu Wakuu wafuatao:

  1. Dkt. Grace Elias Maghembe kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda Wizara ya Afya.
  • Bw. Nicholas Merinyo Mkapa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

E: Uteuzi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi

Mheshimiwa Rais amemteua Bw. Ramadhani Kombwey Kailima kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi. Bw. Kailima, anachukua nafasi ya Dkt. Wilson Mahera Charles ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Viongozi wote walioteuliwa katika nafasi mpya pamoja na Naibu Mawaziri waliohamishwa wizara wataapishwa Jumatatu, tarehe 27 Februari, 2023 Ikulu Chamwino, Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *