TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavYo:-

  1. Amemteua Bw. Andrew Wilson Massawe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI). Bw. Massawe anajaza nafasi ya Dkt. Tausi Mbaga Kida aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Uwekezaji.

Uteuzi huo umeanza tarehe 02 Aprili, 2023; na

  • Amemteua Prof. Ulingeta Obadia Lebson Mbamba kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa kipindi cha miaka mitatu (03). Prof. Mbamba anachukua nafasi ya Prof. Blasius Bavo Nyichomba ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi huo umeanza tarehe 29 Machi, 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *