Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Afuturisha Viongozi pamoja na Makundi Mbalimbali, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Aprili, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Ukumbi wa Kikwete kwa ajili ya Kufutarisha Viongozi pamoja na Makundi mbalimbali, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Aprili. 2023.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Omar wakati wa Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Aprili. 2023.
Viongozi mbalimbali, Wasanii, Wahariri wa vyombo vya Habari pamoja na Wageni wengine wakiwa kwenye ukumbi wa Kikwete kwa ajili ya Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam. Futari hiyo iliandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 15 Aprili 2023.
.
.
.
.
.
.
.
.
Mahasimu wa jadi Simba na Yanga wakutana kwenye Futari Ikulu Jijini Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Rais wa Yanga Eng. Hersi Said, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba Salim Abdallah (Try again) wa pili kutoka kulia pamoja na Mfadhili na Mdhamini wa Yanga Ghalib Said Mohamed wa pili kutoka kushoto wakiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 15 Aprili 2023. Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Mama Janeth Magufuli wakati wakitoka kwenye Futari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Aprili. 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *