Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ashuhudia Utiaji Saini Mikataba Baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni 3 za Uchimbaji Madini Muhimu na Madini ya Kimkakati, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni tatu (3) za Uchimbaji Madini Muhimu na Madini ya Kimkakati kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Eliezer Mbuki Feleshi wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Msingi (Framework Agreement) baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya EcoGraf Limited ya Australia iliyowakilishwa na Mtendaji Mkuu wake Andrew Spinks pamoja na Christer Mhingo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023. Mkataba huu unahusu mradi wa Epanko, Ulanga Mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu akisaini Mkataba wa makubaliano ya Wanahisa baina ya Serikali na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya EcoGraf Limited ya Australia iliyowakilishwa na Mtendaji Mkuu wake Andrew Spinks pamoja na Christer Mhingo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Eliezer Mbuki Feleshi wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Msingi (Framework Agreement) baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Evolution Energy Minerals ya Australia iliyowakilishwa na Mtendaji Mkuu wake Phillip Hoskins, pamoja na viongozi wengine Michael Bourgnoin pamoja na Heavenlight Kavishe kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023. Mkataba huo ni wa Chilalo, Ruangwa Mkoani Lindi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu akisaini Mkataba wa makubaliano ya Wanahisa baina ya Serikali na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Evolution Energy Minerals ya Australia iliyowakilishwa na Mtendaji Mkuu wake Phillip Hoskins, pamoja na viongozi wengine Michael Bourgnoin pamoja na Heavenlight Kavishe kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Eliezer Mbuki Feleshi wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Msingi (Framework Agreement) baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Peak Rare Earth Limited ya Australia iliyowakilishwa na Mwenyekiti Mtendaji wake Russell Scrimshaw wapili (kulia) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bardin Davis kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu akisaini Mkataba wa makubaliano ya Wanahisa baina ya Serikali na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Peak Rare Earth Limited ya Australia iliyowakilishwa na Mwenyekiti Mtendaji wake Russell Scrimshaw wapili (kulia) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bardin Davis kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023. Mkataba huo unahusu Mradi wa Ngualla uliopo Mkoani Songwe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *