TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:

  1. Bw. Amos Gabriel Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  • Bw. Adam Kighoma Malima amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
  • Bi Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
  • Bw. Albert John Chalamila amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Uhamisho huu wa Wakuu wa Mikoa unaanza mara moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *