TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewateua Majaji wa Mahakama ya Rufaa wafuatao:- 

  1. Amemteua Jaji Zainab Goronya Muruke kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Muruke alikuwa Jaji Mfawidhi, Kituo Jumuishi cha Mashauri ya Ndoa, Talaka na Mirathi – Temeke, Dar es Salaam;
  • Amemteua Jaji Dkt. Benhajj Shaaban Masoud kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.  Kabla ya uteuzi huo, Jaji Masoud alikuwa Mkuu wa Shule ya Sheria Tanzania;
  • Amemteua Jaji Amour Said Khamis kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Khamis alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora;
  • Amemteua Jaji Leila Edith Mgonya kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.  Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mgonya alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Masijala Kuu Dar es Salaam;
  • Amemteua Jaji Gerson John Mdemu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mdemu alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma; na
  • Amemteua Jaji Agnes Zephania Mgeyekwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mgeyekwa alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi.

Uteuzi huu wa Majaji wa Mahakama ya Rufani umeanza tarehe 28 Aprili, 2023 na wataapishwa kwa tarehe itakayopangwa baadae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *