Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan apokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Agosti, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Wapigania Uhuru wa Zimbabwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ZANU-PF Mhe. Oppah Chamu Zvipange Muchinguri Kashiri mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Emmerson Mnangagwa tarehe 04 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa uliowasilishwa kwake na Waziri wa Ulinzi na Wapigania Uhuru kutoka Zimbabwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ZANU-PF Mhe. Oppah Chamu Zvipange Muchinguri Kashiri mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mjumbe Malum wa Rais wa Zimbabwe ambaye ni Waziri wa Ulinzi na Wapigania Uhuru na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ZANU-PF Mhe. Oppah Chamu Zvipange Muchinguri Kashiri Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Agosti, 2023. Mhe. Rais Samia ameitakia kheri Zimbabwe katika Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mjumbe Maalum wa Rais wa Zimbabwe ambaye ni Waziri wa Ulinzi na Wapigania Uhuru na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ZANU-PF Mhe. Oppah Chamu Zvipange Muchinguri Kashiri mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Agosti, 2023.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mjumbe Maalum wa Rais wa Zimbabwe ambaye ni Waziri wa Ulinzi na Wapigania Uhuru na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ZANU-PF Mhe. Oppah Chamu Zvipange Muchinguri Kashiri pamoja na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wa tatu kutoka (kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhe. Fatma Mohammed Rajab wa pili kutoka kulia pamoja na viongozi wengine tarehe 04 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mjumbe Maalum wa Rais wa Zimbabwe ambaye ni Waziri wa Ulinzi na Wapigania Uhuru na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ZANU-PF Mhe. Oppah Chamu Zvipange Muchinguri Kashiri mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Agosti, 2023.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *