Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-
- Amemteua Mhe. Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).
- Amemteua Mhe. Anne Semamba Makinda, Spika Mstaafu kuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Ushirika Moshi (MoCU).
Uteuzi huu unaanza mara moja.