TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na utenguzi wa Viongozi mbalimbali kama ifuatavyo:

 1. Amemteua Ndugu Said Othman Yakubu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Yakubu alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
 • Amemteua Ndugu Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo, Ndugu Msigwa alikuwa Mkurugenzi wa Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali. Nafasi iliyoachwa wazi ya Mkurugenzi wa Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali itatangazwa baadae.

MAKATIBU TAWALA MKOA

 • Ametengua uteuzi wa Ndugu Abdallah Mohamed Malela, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara. Badala yake amemteua Bi. Bahati Ibrahim Geuzye kuwa katibu Tawala Mkoa wa Mtwara. Kabla ya uteuzi huu, Bi Bahati alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
 • Amemteua Ndugu Mohamed Jumanne Gombati kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Gombati alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Maafisa Waandamizi katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

WAKUU WA TAASISI

 • Amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Aidha aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Bw. Omar Issa ataendelea na majukumu mengine aliyopangiwa katika Ofisi ya Rais – Tume ya Mipango.
 • Amemteua Ndugu Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Anachukua nafasi ya Mhandisi Peter R. Ulanga ambaye atapangiwa kazi nyingine.
 • Amemteua Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kabla ya uteuzi huu Ndugu Nyamo – Hanga aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
 • Amemteua Dkt. Erasmus Fabian Kipesha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Kipesha alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (TEA).

WAKUU WA WILAYA

 • Ametengua uteuzi wa Ndugu Hanafi Msabaha, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini na badala yake amemteua Bi. Mwanahamisi Mkunda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mkunda aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.
 1. Amemteua Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Mariam Chaurembo atapangiwa kazi nyingine.

WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI (MA -DED)

 1. Amemteua Ndugu Hassan Bakari Nyange kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara TC. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Nyange alikuwa DAS Wilaya ya Namtumbo. Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi (DED) wa Wilaya ya Mtwara TC, Kanali Emmanuel Mwaigobeko atapangiwa kazi nyingine.
 1. Ametengua uteuzi wa Bi. Tatu Said Issike, Mkurugenzi wa Mtwara DC na kumteua Ndugu Abeid Abeid Kafunda kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara DC. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Kafunda alikuwa Mwanasheria katika Ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali.
 1. Amemteua Ndugu Reuben Sixbert Jichabu kuwa Mkurugenzi (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu Erica Yegella atapangiwa kazi nyingine.

KATIBU TAWALA WILAYA

 1. Amemteua Ndugu Francis George Mgoloka kuwa Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) ya Namtumbo. Kabla ya uteuzi huo Ndugu Mgoloka alikuwa Katibu Tarafa Mswaki – Kilindi Handeni.

Katibu Mkuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa siku ya Jumanne saa sita mchana Ikulu, Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *