Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameteua na kuridhia uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:
- Amemteua Bw. Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Regulatory Authority – TFRA).
Kabla ya uteuzi Bw. Laurent alikuwa Mhadhiri, Shule ya Sheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania).
- Ameridhia uteuzi wa Bw. Patrick Magologozi Mongella kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (Cereals and Other Produce Board – CPB). Bw. Mongella ni Mkurugenzi wa Miradi, Benki ya Maendeleo TIB.
- Ameridhia uteuzi wa Bi. Mwanahiba Mohamed Mzee kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (Agricultural Inputs Trust Fund – AGITF). Bi. Mwanahiba aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania.
- Ameridhia uteuzi wa Bi. Irene Madeje Mlola kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na mazao Mchanganyiko (Cereals and Other Produce Regulatory Authority – COPRA). Bi Mlola aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Financial Sector Deepening Trust (FSDT).
- Ameridhia uteuzi wa Dkt. Andrew Marcelin Komba kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (National Food Reserve Authority – NFRA). Bw. Komba ni Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais.
- Ameridhia uteuzi wa Bw. Felix H. Mlaki kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (National Ranching Company Limited – NARCO). Bw. Mlaki ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya NARCO.