Rais Samia Ashiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) Luanda Nchini Angola Tarehe 04 Novemba, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa, Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema, Rais wa Angola Mhe. João Lourenço, Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Félix Tshisekedi pamoja na Viongozi mbalimbali kabla ya kuanza kwa Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika SADC, Luanda nchini Angola tarehe 04 Novemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa (kushoto) Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema (kulia) wakati wakijiandaa kwenda kwenye Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika SADC, Luanda nchini Angola tarehe 04 Novemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa Wimbo wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika SADC pamoja na ule wa Umoja wa Afrika (AU) ukiimbwa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Utangulizi kuhusu Ulinzi na Usalama (Troika) wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC, Luanda nchini Angola tarehe 04 Novemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano kuhusu Ulinzi na Usalama (Troika) wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC, Luanda nchini Angola tarehe 04 Novemba, 2023. Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo utajadili juhudi za SADC katika kuimarisha hali ya Amani, Ulinzi na Usalama Mashariki mwa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *