Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis awasili Ikulu Jijini Dar es Salaam Leave a reply Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtambulisha Mgeni wake Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis kwa viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Mgeni wake Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa katika mapokezi Rasmi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023. Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023 Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni wake Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Ujumbe wa Romania ulioongozwa na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Klaus Iohannis Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam kufuatia Ziara ya Kitaifa ya Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis nchini Tanzania tarehe 17 Novemba 2023 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis wakati wakishuhudia utiaji saini wa Mikataba mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo iliyotiwa saini na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama na Waziri wa nchi wa masuala ya Dunia na Mikakati ya Kidiplomasia wa Romania Mhe. Traian- Laurentiu Hristea kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Novemba 2023.