Rais Samia Suluhu Hassan ashiriki Maadhimisho ya Miaka62 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Kuzindua Mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua Mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Rais Samia alifanya uzinduzi huo wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi wa Mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Rais Samia alifanya uzinduzi huo wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 09 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Lawrence Mafuru pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati ya Uongozi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.
Viongozi, pamoja na wageni mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na uzinduzi wa Mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 9 Desemba, 2023.
Viongozi, pamoja na wageni mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na uzinduzi wa Mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 9 Desemba, 2023.
.
Vijana wa Kwaya ya Utumishi wakiwa kwenye uzinduzi wa Mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 9 Desemba, 2023.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Gilead Teri wakati akielezea majukumu ya Kituo wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *