TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:

 1. Uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa
 1. Amemteua Bi Maryam Ahmed Muhaji kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara. Kabla ya uteuzi huu Bi. Muhaji alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Wanging’ombe. Anachukua nafasi ya Bi. Karoline Albert Mthapula ambaye atapangiwa kazi nyingine.
 • Uteuzi wa Katibu Tawala wa Wilaya
 1. Amemteua Bi. Zuhura Abdulrahman Rashid kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa. Bi. Rashid ni Afisa Mwandamizi katika Mfuko wa Taifa wa Maji. Anachukua nafasi ya Bi. Shamim Sadiq ambaye atapangiwa kazi nyingine.
 • Uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
 1. Amemteua Bw. Michael Kachoma kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega. Bw. Kachoma anachukua nafasi ya Bi. Veronica Vicent Sayore ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
 • Uhamisho wa Wakuu wa Wilaya
 1. Mhe. Mayeka Simon Mayeka amehamishwa kutoka Wilaya ya Chunya kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa.
 1. Mhe. Remidius Mwema Emmanuel amehamishwa kutoka Wilaya ya Kongwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto.
 1. Mhe. Mbaraka Alhaji Batenga amehamishwa kutoka Wilaya ya Kiteto kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya.
 1. Mhe. Kanali Hamis Mayamba Maiga amehamishwa kutoka Wilaya ya Rombo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi.
 • Mhe. Kanali Wilson Christian Sakullo amehamishwa kutoka Wilaya ya Misenyi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro.
 • Mhe. Raymond Stephen Mwangwala amehamishwa kutoka Wilaya ya Ngorongoro kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo.
 • Uhamisho wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri
 1. Bi. Rose Robert Manumba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi.
 1. Bi. Rehema Said Bwasi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
 1. Bw. Yefred Edson Myenzi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita.
 1. Bi Zahara Muhiddin Michuzi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Geita kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara.
 • Bi. Lena Martin Nkya amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Ifakara kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma.
 • Bw. Chiriku Hamis Chilumba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
 • Bw. Kisena Magena Mabuba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
 • Bw. Simon Sales Berege amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji.
 1. Bw. Michael John Gwimile amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
 • Bi. Regina Lazaro Bieda amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Momba kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
 • Bi. Mwajuma Abasy Nasombe amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
 • Bw. Rashid Karim Gembe amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga.
 • Bi. Zahara Abdul Msangi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga.
 • Bw. Philemon Mwita Magesa amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Tunduma kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
 • Bi. Butamo Nuru Ndalahwa amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba.

Uteuzi na uhamisho huu umeanza tarehe 12 Desemba, 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *