Category Archives: Top Stories

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam Bw. Aron Titus Kagurumjuli.

Mhe. Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo tarehe 16 Februari, 2021.

Uteuzi wa Mkurugenzi mwingine wa Manispaa hiyo utafanywa baadaye.

Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya picha ya Wanyama watano (The Big Five) mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa SADC Mhe. Filipe Jacinto Nyusi mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita.