Author Archives: Ikulu Ikulu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 02 Juni, 2021 amemuapisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (KaziMaalum) Mhe. Kept. Mst. George Huruma Mkuchikaaliyemteua tarehe 31 Machi, 2021 na amewaapishaMakatibu Tawala wa Mikoa 11 aliowateua tarehe 29 Mei, 2021.

Hafla ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoahao imefanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma nakuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim MajaliwaMajaliwa na Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson.

Makatibu Tawala wa Mikoa walioapishwa ni Mhe. Balozi Batilda Salha Buriani (Shinyanga), Bw. Rodrick Lazaro Mpogolo (Katavi), Bi. Dorothy Aidan Mwaluko(Singida), Dkt. Athumani Juma Kihamia (Arusha), Mhandisi Mwanaisha Rajabu Tumbo (Pwani), Bw. Ngusa Dismas Samike (Mwanza), Bw. Hassan Abasi Rugwa (Dar es Salaam), Dkt. Fatuma Ramadhan Mganga(Dodoma), Bw. Musa Ramadhani Chogero (Geita), Bi. Pili Hassan Mnyema (Tanga) na Bi. Prisca Joseph Kayombo(Simiyu).

Mhe. Rais Samia ameshuhudia Makatibu Tawala waMikoa hao pamoja na Wakuu wa Taasisi 4 aliowateuahivi karibuni wakila kiapo cha uadilifu kwa watumishiwa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jajiwa Mahakama ya Rufani Mhe. Sivangilwa SikalalilwaMwangesi. Wakuu wa Taasisi hao ni Mkurugenzi waUpelelezi wa Makosa ya Jinai CP. Camilius Wambura, Mkuu wa Kamisheni ya Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi CP. Hamad Khamis Hamad, Afisa MtendajiMkuu, Tume ya Ushindani wa Biashara Bw. William Erio na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwaWafanyakazi Dkt. John Kedi Mduma.

Akizunguza katika hafla hiyo, Mhe. Rais Samiaamewapongeza viongozi wote walioapishwa naamewataka kwenda kuchapa kazi kwa juhudi, maarifa, kuzingatia sheria na utu ili kutimiza matarajio yawananchi kwa Serikali yao.

Mhe. Rais Samia amewataka Makatibu Tawala waMikoa kutekeleza ipasavyo wajibu wao wa kuwa kiungokati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, kusimamiavizuri rasimali za umma hasa ukusanyaji wa mapato namatumizi yake, kuhakikisha mapato yanayopaswakuelekezwa katika shughuli za maendeleo na makundimaalumu yanapelekwa kama ilivyopangwa katikahalmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji.

Ameonya dhidi ya vitendo vya baadhi ya viongozikudharauliana, kubaguana, kurumbana na kugombanabadala ya kushirikiana kusukuma mbele maendeleo yaMikoa na taasisi wanazoziongoza pamoja na kutatuakero na malalamiko ya wananchi.

Pia, ametaka viongozi hao kwenda kushughulikiamigogoro inayowakabili wananchi hususani migogoroya mirathi ambayo inawaathiri zaidi wanawake, migogoro ya ardhi na ameonya kuwa hatavumiliakuona viongozi hao wanakuwa sehemu ya migogorokutokana na kujimilikisha ardhi katika maeneowanayoongoza.

Mhe. Rais Samia amewataka Makatibu Tawala waMikoa kushughulikia changamoto zinazowakabiliwatumishi wa umma, kusimamia uchumi vizuri ikiwa nipamoja na kusimamia uendelezaji wa viwanda, kuvutiawawekezaji, kusimamia vizuri taasisi za Serikali zilizopokatika Mikoa yao, kusimamia kwa ukaribu miradi yamaendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao nakushirikiana na wananchi na Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika utekelezaji wa Ilani iliyoiweka Serikalimadarakani.

Aidha, Mhe. Rais Samia amewaonya viongozi haopamoja na viongozi wengine walioteuliwa katikanyadhifa mbalimbali kuacha vitendo kwendaMajimboni kufanya kampeni za chinichini za kutakaUbunge na badala yake wawaache Wabunge waMajimbo hayo kutumikia wananchi kwa amani mpakawakati wake ukifika.

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akagua ujenzi wa Barabara ya Mwendokasi ya Mbagala tarehe 01 Juni, 2021

Wananchi wa Mtongani na Kwa Azizi Ali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasalimia wakati akikagua ujenzi wa Barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) Awamu ya Pili (Mwendokasi) katika barabara ya Kilwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mbagala, Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi katika barabara ya Kilwa.

Wananchi wa Mbagala wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza nao wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi katika barabara ya Kilwa.