Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye Uwanja wa Kololo jijini Kampala kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassani Mwinyi kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Mwinyi alihudhuria pia sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Kikwete pia alihudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa mataifa mbalimbali katika viwanja vya Kololo jijini Kampala.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa viongozi wa dini wa Taifa la Uganda katika viwanja vya Kololo jijini Kampala.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa wa Sudani Kusini Salva Kir mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya tukio la uapisho.