Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi watatu kutoka (kulia), Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wanne kutoka (kulia) watatu kutoka kushoto, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wanne kutoka (kushoto), Mtendaji mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Elius Mwakalinga wakwanza (kulia) Pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga wakwanza kushoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara. Hosteli hizo zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 3840 na ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa hosteli za wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hosteli hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA Elius Mwakalinga akitoa ufafanuzi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa Hosteli hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga tumba katika bendi ya Msondo Ngoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mke wake Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wakipiga makofi wakati brass bendi ya JKT ilipokuwa ikitumbuiza mara baada ya kukamilika kwa tukio la kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati akiwasili katika viwanja vya hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Taaswira ya moja ya moja ya hosteli hizo za wanafunzi ambazo ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu