Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. John Kiang’u Jingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Azizi Mlima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Kiang’u Jingu wa kwanza kulia, akifatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Azizi Ponary Mlima pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya wakila Kiapo cha Uadilifu mara baada ya kuapishwa katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Kiang’u Jingu wa kwanza kulia, akifatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Azizi Ponary Mlima pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya waki tia saini kwenye hati ya Uadilifu katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya akizungumza mara baada ya kuapishwa katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya tukio la Uapisho lililofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU Diwani Athuman Msuya pamoja na Balozi mteule Valentino Mlowola mara baada ya tukio la Uapisho katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Kamishna wa kupambana na madawa ya kulevya Rogers Sianga, katika kipindi kinachorushwa na azam TV chini ya ndugu Tiddo Mhando amesema suala la madawa ya kulevya halipo kwa viongozi wa serikalini.
Binafsi kauli hii ya Kamishna huyu imenistua sana kwani haiwezekani kusema kiujumla tu kwamba eti viongozi wa serikali hawajihusishi na madawa ya kulevya.
Nini kimejificha nyuma ya pazia juu ya kauli hii? Kwa hiyo kumbe wanaohusika na madawa ya kulevya ni wanasiasa wa upinzani, wasanii na wafanyabiashara tu! Kwa staili hii vita ya kupambana na madawa ya kulevya haitokuja kufanikiwa.
Kamishna Rodgers anasema hakuna connection yoyote ya viongozi wa serikali kujihusisha na madawa ya kulevya. Hebu tujiulize kama tu ndo ameteuliwa hajafanya kazi hata wiki tatu then anakuja anasema hajaona connection ya viongozi wa serikali kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Hii inaleta picha gani?
Nasi tutafuatilia ili kujiridhisha Ukweli wa kauli hiyo