RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO-BUSISI LINALOUNGANISHA WILAYA YA MISUNGWI NA SENGEREMA MKOANI MWANZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine akivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kutoka Kigongo hadi Busisi lenye urefu wa km 3.2 katika sherehe zilizofanyika katika eneo la Kigongo Misungwi mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Daraja hilo refu kupita yote katika ukanda wa Afrika Mashariki lenye urefu wa km 3.2 katika sherehe zilizofanyika katika eneo la Kigongo Misungwi mkoani Mwanza.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia picha ya mfano wa Daraja hilo litakalojengwa kutokea Kigongo Misungwi hadi Busisi Sengerema mkoani Mwanza. Daraja hilo litakalopita ziwani litakuwa na urefu wa km 3.2 na kufanya kuwa Daraja refu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Daraja hilo la kutoka Kigongo hadi Busisi mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Kigongo na Busisi mara baada ya kuwasili katika eneo la mradi wa ujenzi wa Daraja hilo refu.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Daraja la kutoka Kigongo hadi Busisi Misungwi mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Inseni B iliyopo Kata ya Butimba mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati akiwa na Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Iseni B Salma Yasin ambaye alielezea vizuri kero mbalimbali za Shule yao na kufanikiwa kuchangiwa kiasi cha Shilingi milioni 5 na Mhe. Rais Dkt. Magufuli. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati akiwa na Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Iseni B Salma Yasin ambaye alielezea vizuri kero mbalimbali za Shule yao na kufanikiwa kuchangiwa kiasi cha Shilingi milioni 5 na Mhe. Rais Dkt. Magufuli. 

Mbunge wa Misungwi Mhe Charles Kitwanga akishiriki kwenye ngoma
ya utamaduni ya kucheza na nyoka mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa sherehe ya  uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi  lenye urefu wa Kilomita 3.2 kwenye sherehe iliyofanyika Kigongo jijini Mwanza. Desemba 7, 2019

Picha iliyotengenezwa kwa computer ya namna daraja la Kigongo – Busisi litakavyokuwa mara baada ya kukamilika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *