RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA SOKO KUU LA MKOA WA MOROGORO NA KULIITA SOKO LA CHIFU KINGALU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare wakati wakifungua utepe kuashiria kufungua Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro leo tarehe 11 Februari 2021 mkoani Morogoro.
Muonekano wa Soko kuu la chifu Kingalu wa Morogoro lililo funguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare leo tarehe 11 Februari 2021 mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakatiakikata utepe kufungua Soko Kuu la Chifu Kingalu, Morogoro pamoja na Waziri waTamisemi Selemani Jafo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare, Mbunge wa Morogoro mjini Aziz Abood pamoja na viongozi wengine wa mkoa wa Morogoro leo Februari 11 ,2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza kero mbalimbali za wafanyabiashara wa Soko Kuu la chifu Kingalu mkoa wa Morogoro ili kujua changamoto zao mara baada ya kulifungua Soko hilo katika Manispaa ya Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanya biashara mbalimbali wa Soko Kuu la mkoa wa Morogoro ili kujua changamoto zao mara baada ya kulifungua Soko hilo katika Manispaa ya Morogoro.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo ,na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba ,wakati alipowataka kujibu kero na malalamiko yaliyotolewa na wafanyabiashara wa soko kuu la Chifu Kingalu Morogoro kuhusu changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza kumsikiliza baada ya kutoka kuzindua soko kuu la Chifu Kingalu Morogoro leo Februari 11 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kutoka kuzindua soko kuu la Chifu Kingalu ambapo amesisitiza viongozi kuwajibika na kutatua matatizo na kero za wananchi aidha amesisitiza kuondolewa kwa tozo za ushuru wa mazao kwa wafanya biashara kwa mzigo usio zidi Tani moja , “Serikali yangu iliamua kufuta kodi hizi ili kuwaondolea mateso wananchi hawa wanao hangaika kujipatia riziki, Wakurugenzi wa Manispaa mnatakiwa kuheshimu sheria hii na sivinginevyo msijiundie sheria ndogo ndogo (ByLaws ), tafuteni vyanzo vingine vya mapato kodi ya Pango ya vizimba wanayowalipa ni sawa , Mkaheshimu sheria hii ilipitishwa na Bunge hakuna ushuru kwa mzigo usiozidi tani moja sokoni, sasa nakuagiza Waziri wa Tamisemi kuhakikisha sheria hii inatekelezeka” , alisema Mhe. Rais Magufuli, Morogoro leo Februari 11, 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *