Mhe Rais Samia Hassan Suluhu afanya uteuzi..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi 4 kama ifuatavyo;
Kwanza, Mhe. Rais Samia amemteua Dkt. Florencs Turuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma.
Dkt. Turuka anachukua nafasi ya Dkt. Charles Msonde ambaye amemaliza muda wake.
Pili, Mhe. Rais Samia amemteua Mhandisi Dkt. Richard Masika kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (Tanzania Engineering and Manufacturing Design Organization – TEMDO).
Dkt. Masika anachukua nafasi ya Prof. Patrick Makungu ambaye muda wake umekwisha.
Tatu, Mhe. Rais Samia amemteua Dkt. Blandina Robert Lugendo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Fisheries Education and Training Agency – FETA).
Nne, Mhe. Rais Samia amemteua Bi. Paulina Mbena Nkwama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (Teacher’s Service Commission).
Kabla ya uteuzi huo, Bi. Nkwama alikuwa Katibu Tawala Msaidizi (Elimu) Mkoa wa Kilimanjaro na anachukua nafasi ya Bi. Winfrida Rutaindurwa ambaye amemaliza muda wake.
Uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 29 Machi, 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *