






Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshiriki Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ,NEC ambayo yeye ni mjumbe . Mkutano huu umefanyika Makao Makuu ya CCM White House jijini Dodoma, agenda Kuu ikiwa ni kufanya uteuzi wa kujaza nafasi za uongozi ndani ya Chama zilizo wazi kwa sababu mbalimbali, kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama utakaowathibitisha , kesho tarehe 30 April 2021.