Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wanne wanaoziwakiklisha nchi zao hapa Tanzania.Mabalozi walioziwasiliasha hati zao leo ikulu ni pamoja na Hawa Ndilowe- Malawi,Jasem Ibrahim Al- Najem- Kuwait, Thamsanqa Dennis Mseleku-Afrika ya Kusini na Chirau Ali Mwakwere- Kenya.Pichani Mabalozi hao wakiwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Balozi Ndilowe akiwa na Rais Kikwete akifanya naye mazungumzo baada ya kuwasilisha hati za utambulisho.
Balozi mpya wa Kuwaiti nchini Tanzania Mhe.Jasem Ibrahim Al-Najem akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete hati za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam February 18, 2015
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania akiwa katika picha na Rais Dkt.Jakaya Kikwete na wakiwa katika mazungumzo baada ya kuwasilisha hati za utambulisho.
Balozi Mpya wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania Mhe.Thamsanqa Dennis Mseleku akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam February 18, 2015. Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na balozi mpya wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania Thamsanqa Dennis Mseleku baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho na kufanya naye mazungumzo
Balozi Mpya wa Kenya nchini Tanzania Mhe.Chirau Ali Mwakwere akiwasilisha Kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam February 18, 2015. Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania Chirau Ali Mwakwere wakikumbatiana na kwa furaha muda mfupi baada ya balozi huyo kuwasilisha hati zake za utambulisho ikulu jijini Dar es Salaam