ZIARA YA RAIS JAKAYA KIKWETE MKOANI RUVUMA WILAYA YA NAMTUMBO

ANGALIA RAIS ALIVYOFUNGUA BARABARA YA AMTUMBO SONGEA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI  KUZINDUA RASMI UJENZI WA BALABALA YA LAMI YA NAMTUMBO – MATEMANGO YENYE UREFU WA KILOMITA 128.9 MKOANI RUVUMA JULAI 21,2014

 

china

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Balozi Mdogo wa Japan Bwana Kazuyoshi Matsunaga(katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(African Development Bank) ADB Bibi Tonia Kondiero kulia wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Lami ya Namtumbo- Matemanga  yenye urefu wa kilomita 128.9 uliofanyika katika kijiji cha Migelegele Julai 21,2014 .Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli na watatu kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Barabara hiyo inajengwa na serikali ya Tanzania ikisaidiwa na fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika na serikali ya Japan kupitia shirika lake la misaada la JICA.

D92A7678

Rais Dkt.Jakaya Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za millennia(Millenium Challenge Corporation Bwana Karl Fickensher wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi Kuzindua Barabara ya Lami ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa kilometa 71.4 iliyojengwa kwa msaada wa Watu wa Marekani kupitia mfuko huo wakati wa hafla iliyofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo julai 21,20142 (1)  4 (2)

Rais Dkt.Jakaya Kikwete  alipanda mti wa kumbukumbu wa uzinduzi wa Barabara ya Lami ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa kilometa 71.4 iliyojengwa kwa msaada wa Watu wa Marekani kupitia mfuko huo wakati wa hafla iliyofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo na  ujenzi wa Barabara ya Lami ya Namtumbo- Matemanga  yenye urefu wa kilomita 128.9 uliofanyika katika kijiji cha Migelegele Julai 21,2014 

D92A7986

 Rais Dkt.Jakaya Kikwete  akifungua kitambaa kufungua rasmi Hospital ya Wilaya ya  Namtumbo  Julai 21,2014

12 (2)

Rais Dkt.Jakaya Kikwete  akikagua vyumba vya kutolea huduma ya Afya katika Hospital hiyo baada ya kuifungua  rasmi Hospital ya Wilaya ya  Namtumbo  Julai 21,2014

  ambiolase

Moja ya ambulance inayotumika kwa ajili ya kubebea wagonjwa toka sehemu mbalimbali kuwapeleka Hosipitalini hapo kwa ajili ya huduma ya Afya

D92A7978

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wauguzi wa wa Hospital ya Wilaya ya  Namtumbo  baada ya kuifungua rasmi Hospitali hiyo Julai 21,2014 D92A7268Mtoto Gloria Fusi mwenye umri wa miaka saba anayesoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Utwango wilayani Namtumbo akiandika jina lake katika Notebook ya Mama Salma Kikwete wakati Rais Kikwete aliposimama katika kijiji cha Utwango kuwasalimia wananchi akiwa njiani kuelekea mjini Namtumbo akitokea Songea mjini. Mtoto Gloria alimsalimia Mama Kikwete kwa uchangamfu na ndipo Mama Salma alipomuuliza kama anajua kuandika jina lake na hivyo kumpatia notebook yake na mtoto huyo bila kusita aliandika vizuri jina lake Julai 21,2014 D92A8180  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia Mzee Mustafa Mangunyuka muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo wa taifa wilayani Namtumbo ambapo aliwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara Julai 21,2014

KILEMA Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kiwete akiteta jambo na mkazi wa kijiji cha Ligela wilayani Namtumbo Bwana Edwin Ngonyani wakati alipokuwa anahitimisha ziara yake wilayani humo.Bwana Ngonyani ambaye alipata ulemavu baada ya kupoteza miguu yote miwili katika ajali ya moto alimweleza Rais kuwa anapata taabu ya kutafuta riziki kwa kuwa anatambaa kwa taabu.Rais Kikwete alitoa ahadi ya kumsaidia mlemavu huyo ili aweze kujikimu kimaisha

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *