Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amir Jeshi Mkuu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, April 26, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amir Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam April 26, 2015
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amir Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa na kupokea heshima ya mizinga 21 katika Sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam Aprili 26, 2015
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amir Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifuatilia kwa karibu sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam April 26, 2015 . Kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange
Vikosi vya ulinzi na usalama vikitoa heshima mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amir Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika Sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam Aprili 26, 2015
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake , wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam April 26, 2015