Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum alipowasili kwenye makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda (nyuma yao) Oysterbay jijini Dar es salaam kwa ajili ya Futari leo Jumamosi Julai 26, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na wa pili kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova
Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakijumuika na waumini wengine katika Swala ya Magharibi katika makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda Oysterbay jijini Dar es salaam alikoandaa Futari leo Jumamosi Julai 26, 2013
Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ndg Ramadhani Madabida wakipakua futari
Mawaziri wakuu Wastaafu Mzee Cleopa Msuya na Jaji Joseph Sinde Warioba wakiwa wameketi pamoja na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu (kulia, mwenye baraghashia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio
Meza kuu ikifurahia jambo baada ya futari
Rais Kikwetena Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakisalimiana na waalikwa
Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wazee mashuhuri wa Dar es salaam
Rais Kikwete akisalimiana na mchora katuni maarufu Ali Masoud ‘Kipanya’ huku Mrisho Mpoto akisubiri zamu yale
Mkono wa mwisho ni wa mtoto huyu aliyepata bahati ya kuagana na Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali baada ya futari pamoja na mwenyeji waziri mkuu Mizengo Peter Pinda