Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes na viongozi wa chuo kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes na viongozi wa chuo wakipata maelezo kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viogozi wa chuo jukwaa kuu wakisimama wakati nyimbo za Taifa za Tanzania na Australia zikipigwa wakati wa kuanza kwa sherehe za kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
wasanii wa kabila la Wakakulang wakicheza ngoma za asili yao katika kunogesha sherehe za kihistorua ambapo Rais Kikwete amekuwa ni Mkuu wa Nchi wa kwanza kupokea digrii hiyo ya heshima kutoka katika Chuo hicho.
RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA SHERIA (DOCTOR OF LAWS HONORIFIC CAUSA) NA CHUO KIKUU CHA NEWCASTLE .
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Chuo Kikuu cha Newcastle cha nchini Australia.
Sherehe za kumtunuku Rais shahada hiyo zimefanyika leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Newcastle.
Akisoma maelezo ya utangulizi katika hafla hiyo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans amesema Rais Kikwete ni Mkuu wa Nchi wa kwanza kupokea digrii hiyo ya heshima kutoka katika Chuo hicho.
Mkuu huyo wa Chuo amesema Rais Kikwete ametunukiwa shahada hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya duniani si kwa Tanzania tu bali kwa Dunia nzima kwani mchango wake umetambulika na mashirika mbalimbali ya kimataifa yakiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Benki ya Dunia kwa ujumla.
“Tangu kuingia madarakani Rais Kikwete amechangia katika kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu , uchumi na Afya” amesema Bw. Jean na kuongeza kuwa “utawala wake umethibitishia sio Chuo cha Newcastle pekee bali pia kuonesha kanuni ya Msingi kuwa Elimu ni muhimu katika kukuza uchumi, uvumbuzi na katika maendeleo ya jamii” amesisitiza.
Tanzania imekua ikipokea misaada ya elimu kutoka Australia katika nyanja mbalimbali zikiwemo za madini, fedha, habari na tafiti mbalimbali ambazo zimeleta mabadiliko chanya katika jamii na duniani kwa ujumla.
Kwa sasa Watanzania wanne wanachukua masomo ya uzamifu katika masuala ya elimu na siasa.Tayari Watanzania 45 wamemaliza digrii na pia wapo watafiti kutoka Newcastle wanaofanya tafiti zao nchini Tanzania katika masuala ya elimu, afya na uhandisi.
Rais Kikwete ameshukuru na kuelezea jinsi alivyoguswa na tukio hilo ambapo ameushukuru uongozi wa Chuo hicho kwa kutambua mchango wake ambao ameelezea kuwa ameufanya wakati wa kipindi cha uongozi wake kwa moyo, upendo na nia njema kwa wananchi wote wa Tanzania na Dunia kwa ujumla.
“Ilikua nia yangu na wajibu wangu mkubwa kutumia ahadi nilizo waahidi wa Tanzania na hata zaidi ya kile nilicho ahidi na kuelezea kuwa mafanikio haya yote yamechangiwa pia kwa kiasi kikubwa na misingi imara iliyowekwa na viongozi walionitangulia upande wa Tanzania bara na Tanzania Visiwani kwa ujumla”
Katika utawala wake Rais Kikwete ametunukiwa shahada za heshima kutoka vyuo mbalimbali vya Marekani, Canada, China, Uturuki na Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam.
Rais Kikwete pia ametunukiwa tuzo za heshima mbalimbali katika masuala ya Kijamii (United Nations Social Good Award), Afya, Technolojia na Maendeleo (South-South Award for Global Health, Technology and Development) pamoja na Demokrasia (Icon of Democracy Award (Nertherlands)
Rais pia amepata kutunukiwa na kutambuliwa kwa Mchango wake ambapo alitunukiwa nishani kadhaa zikiwemo;
1. (Most Excellent Order of the Peral of Africa) ambayo ni nishani ya juu nchini Uganda.
2. The order of the Green Crescent of the Comoros (Comoros)
3. Order of Abdulazizi Al Saud (Saudi Arabia)
4.Order of excellence (Jamaica)
5. Order of Oman (Oman)
6. AAI African National Achievement Award
7. U.S. Doctors for Africa Award
8. Good Governance in Africa 2015
Sherehe hiyo imehudhuriwa na Mstahiki Meya wa mji wa Newcastle, Mama Nuatali Nelmes, walimu na wakufunzi wa Chuo cha Newcastle, wanafunzi wa Kitanzania na familia zao pamoja na Watanzania kadhaa wanaoishi na kufanya kazi katika mji wa Newcastle.
Rais Kikwete amekamilisha ziara yake ya Kiserikali ya siku nne nchini Australia na anatarajia kuelekea Dar-es Salaam tarehe 30 Julai, 2015
………..Mwisho……….
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Newcastle-Australia
29 Julai, 2015