Monthly Archives: January 2018

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ASALI IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO JIJINI DAR ES SALAAM JANUARI 28,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru mara baada ya kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru kwa kusali pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa mara baada ya wote kwa pamoja kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli. Ibada hiyo ya Jumapili ilifanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Wanakwaya kutoka Chuo cha Ardhi jijini Dar es Salaam wakiimba kwenye Ibada hiyo ya Jumapili ilifanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili na Mke wake Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

 

Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Fr. Asis Mendokta akihubiri katika Ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka Kanisani pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli mara baada ya Ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Nakala za CD ya kwaya kutoka Chuo cha Ardhi mara baada ya Ibada. Kushoto ni Mke wake Mama Janeth Magufuli akifurahia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Kalenda mara baada ya kupewa na moja ya Waumini wa Kanisa hilo mara baada ya Ibada ya jumapili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na waumini wengine mara baada ya ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AAGANA NA BALOZI WA ZIMBABWE ALIYEMALIZA MUDA WAKE NA KUPOKEA UJUMBE MAALUMU WA RAIS WA RWANDA MHE.PAUL KAGAME IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.JANUARI 25,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Zimbabwe aliyemaliza muda wake nchini Mhe. Edzai A.C. Chimonyo aliyefika kumuaga rasmi Ikulu jijini Dar es salaam Januari 25, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Balozi wa Zimbabwe aliyemaliza muda wake nchini Mhe. Edzai A.C. Chimonyo aliyefika kumuaga rasmi Ikulu jijini Dar es salaam Januari 25, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mgeni wake kabla ya kuagana nae Balozi wa Zimbabwe aliyemaliza muda wake nchini Mhe. Edzai A.C. Chimonyo aliyefika kumuaga rasmi Ikulu jijini Dar es salaam Januari 25, 2018

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea  na Dkt Donald Kaberuka, Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame (kushoto kwa Rais),  katika mazungumzo yaliyohudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Mhe. Dotto James na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Profesa Adolf Mkenda Ikulu jijini Dar es salaam 25, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Dkt. Donald Kaberula, Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame  na ujumbe wake pamoja na  na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango,  Mhe. Dotto James na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Uwekezaji Profesa Adolf Mkenda Ikulu jijini Dar es salaam Januari 25, 2018.