Monthly Archives: July 2019

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AZINDUA NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI WA JESHI LA POLISI MKOANI GEITA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugora watatu kutoka kulia, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, Wabunge pamoja na Viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi katika eneo la Magogo mkoani wa Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro wakati akitoka kukagua moja ya nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.

Makamishna kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini wakifurahia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za uzinduzi wa Nyumba za makazi ya Askari Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.

Bendi ya Jeshi la Polisi ikitumbuiza katika sherehe za uzinduzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita.

Sehemu ya Mradi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita ambao umezinduliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Magogo mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Geita mara baada ya kuhutubia katika uzinduzi wa nyumba hizo za makazi ya Askari Polisi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Geita wakati akielekea kuzindua nyumba za Askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Katoro na Buseresere hawaonekani pichani wakati akielekea Geita mjini.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bwanga wakati akitokea Chato mkoani Geita. 

RAIS WA UGANDA MHE. YOWERI KAGUTA MUSEVENI AWASILI CHATO MKOANI GEITA NA KUPOKEWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshma iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya Ngoma na Kwaya mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.

Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni akizungumza na Wananchi wa Chato mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni wakati akiwapungia mkono wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Chato.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni wakati waliupokuwa wakiwasalimia wananchi wa Njiapanda Chato mkoani Geita. 

Sehemu ya Wananchi wa Chato waliojitokeza katika mapokezi ya Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao Chato mkoani Geita. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati akiagana na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja Chato mkoani Geita.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na wananchi wa Nyabilezi kabla ya kuondoka na kurejea nchini kwake Uganda. Rais Museveni ameahidi kujenga madarasa saba kwa ajili ya Shule ya Msingi Nyabilezi Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati akielekea kupanda ndege mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja Chato mkoani Geita.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia kwaya ya watoto wa Shule ya Msingi Kalembo Umitashunta mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kwaya pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati akimsindikiza .