Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibara Dkt. Mohhamed Shein kabla ya mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimfafanulia jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya mazishi ya Kaka yake Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wakimsikiliza kwa Makini Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifafanua jambo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye kaburi la Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga Mkoani Pwani. Mzee Selemani Kikwete alikuwa kaka mkubwa wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Marchi 5,2016
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia baada ya mazishi ya kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, aliyezikwa kijijini kwao Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani Machi 5, 2016