RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA MAJENGO YA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA PAMOJA NA MIRADI MINGINE YA JESHI HILO MKOANI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene, Kamishna Jenerali wa Magereza CGP Suleiman Mzee pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu vya Vyombo vya Ulinzi na Usalama, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa nyumba 24 za makazi ya Maafisa na Askari Magereza katika eneo la Gereza la Isanga mkoani Dodoma leo tarehe 04 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene wakati akiweka jiwe la Msingi ujenzi wa Kiwanda cha Samani cha Jeshi la Magereza Msalato mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Maafisa na Askari Magereza mara baada ya kufungua Majengo ya Makao Makuu ya Jeshi hilo Msalato mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua baadhi ya Mashine ambazo zimeanza kufungwa katika Kiwanda hicho cha Samani cha Magereza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Picha ya Pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Goerge Simbachawene na Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishina Jenerali Suleiman Mzee na Maafisa na Askari wa magereza baada ya kumaliza kufungua nyumba 24 za askari zilizopo eneo la Gereza la kisanga ,Uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha Samani na uzinduzi wa Majengo ya makao makuu ya Jeshi la Magereza eneo la Msalato jijini Dodoma leo Tarehe 4 Februari 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *