Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Julai 23,2015 ameagana na mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania baada ya kumaliza muda wao wa kazi .
Mabalozi walioagana na Rais Julai 23,2015 Ikulu jijini Dar es Salaam ni pamoja na Mhe.Debnath Shaw wa India,Balozi Koenraad Adam wa Ubelgiji na balozi Lennarth Hjelmaker wa Sweden.
Pichani
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi wa India anayemaliza muda wake Mhe.Debnath Shaw wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga ikulu jijini Dar es Salaam julai 23, 2015
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi Koenraad Adam wa Ubelgiji ikulu jijini Dar es Salaam julai 23, 2015 alipokwenda kumuaga. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Sweden nchini aliyemaliza muda wake Mhe.Lennarth Hjelmaker ikulu jijini Dar es Salaam julai 23, 2015