RAIS KIKWETE AFUNGUA BARABARA YA NDUNDU-SOMANGA KILWA MKOANI LINDI AGOSTI 7, 2015

3

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli(wapili kushoto),Balozi wa Kuwaiti nchini Tanzania Mhe.Jassem Ibrahim Al Najem(kulia) pamoja na mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait Bwana Abdulrahman Al Hashim(wapili kulia) wakifunua kitambaa katika jiwe kuashiria kufungua rasmi barabara ya kilometa 60 ya Ndundu-Somanga wakati wa hafla ikiyofanyika katika kijiji cha Marendego Wilaya ya Kilwa leo.Barabara hiyo imefadhiliwa na mfuko wa Kuwait. 

4Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Mwakirishi wa Mfuko wa Kuwaiti Bwana Abdurahman Al Hashim, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe.Jassem Ibrahim Al Najem wakikata utepe kufungua rasmi Barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilomita 60 katika hafla iliyofanyika katika kijiji cha Marendego Wilaya ya Kilwa.Barabara hiyo imejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Kuwaiti.Wengine katika picha ni  mkuu wa mkoa wa Lindi Mwantum Mahiza,Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.  

2Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa sherehe ya ufunguzi wa Barabara ya Ndundu Somanga 

1Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mwakilishi wa mfuko wa Kuwait Bwana Abdulrahman Al Hashim wakati wa sherehe ya ufunguzi wa Barabara ya Ndundu-Somanga iliyofadhiliwa na mfuko huo.Kulia ni Balozi wa Kuwaiti nchini Tanzania Mhe.Jassem Ibrahim al Najem 6Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalamiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe ya ufunguzi wa Barabara ya Ndundu Somanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *