Daily Archives: October 13, 2014

RAIS KIKWETE AZINDUA KIJIJI CHA MFANO CHA VIJANA (PATHFINDERS GREEN CITY) SIKONGE MKOANI TABORA OKTOBA 13,2014

1

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa kijiji cha mfano cha vijana Pathfinders Green City katika kata ya Igigwa wilayani Sikonge Oktoba 13. 2014. Rais Kikwete yupo Mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ambapo pia atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha mbio za mwenge hapo kesho Oktoba 14, 2014. watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bi.Fatma Mwassa na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Bi.Hanifa Selenga.

2

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya uchakataji asali kutoka kwa mmoja wa vijana waishio katika kijiji cha mfano cha vijana wajasiriamali (Pathfinders Green City) katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge, Mkoani Tabora Oktoba 13. 2014

3

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya madawati yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana wajasiriamali katika kijiji cha mfano cha Pathfinders Green City katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge,Mkoani Tabora muda mfupi baada ya kukizindua kijiji hicho.

4

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya madawati yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana wajasiriamali katika kijiji cha mfano cha Pathfinders Green City katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge,Mkoani Tabora muda mfupi baada ya kukizindua kijiji hicho.

5

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na vijana wajasiriamali katika kijiji cha Pathfinders Green City, Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora Oktoba 13. 2014

 

FUATILIA KWA KUANGALIA VIDEO YA MAKALA, RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE ALIVYOPONGEZA KUANZISHWA KIJIJI CHA MFANO PATHIFINDER GREEN CITY TABORA OKTOBA 13, 2014