Monthly Archives: November 2014

RAIS KIKWETE AWASILI DAR ES SALAAM, APATA MAPOKEZI MAKUBWA AKITOKEA NCHINI MAREKANI KWENYE MATIBABU NOVEMBA 29, 2014

8

 

7

 

6

 

5

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea  Marekani kwenye matibabu  Novemba 29, 2014

11

 

9

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014

13

 

12

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014

3

 

4ssss

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu Novemba 29, 2014

14

 

15

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongea na Mama Maria Nyerere aliyefika kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu Novemba 29, 2014
17

 

16

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014

19

 

 

20

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu
22

 

21mmmm

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mashada ya maua kutoka kwa wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu.Novemba 29,2014

1deff

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

2

Mjukuu wa Rais Kikwete Aziza Ridhiwani Kikwete akimpokea kwa shangwe na kadi Babu yake na kisha kupiga naye soga mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam leo akitokea nchini Marekani kwa matibabu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

RAIS OBAMA AMTUMIA SALAMU ZA KHERI RAIS KIKWETE NOV 24, 2014

3334r26we

 

 

unnamed-2

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete salamu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama Nov 24, 2014 jijini BaltimoreMaryland, Marekani.unnamed-7

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na  baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington D.C. wakati walipomtembelea mjini Baltimore Maryland ambapo balozi Liberata Mulamula aliwasilisha kwa Rais Kikwete Salamu maalum za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama Nov 24, 2014 jijini Baltimore,Maryland, Marekani.
rr222222

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington D.C. wakati  walipomtembelea mjini Baltimore Maryland ambapo balozi Liberata Mulamula aliwasilisha kwa Rais Kikwete Salamu maalum za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama Nov 24, 2014 jijini Baltimore, Maryland, Marekani.

 

                      TARATIBU  ZA  TIBA  ZA  RAIS ZAKAMILIKA

unnamed-6

Taratibu za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.

Taratibu hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.

Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani. 

Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.

Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014. 

Rais Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake. 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.

24 Novemba,2014