WATANGAZA nia Kuomba Chama Cha Mapinduzi CCM kuwachagua katika kugombea kiti cha urais mwezi Oktoba 2015 Dkt. John Pombe Magufuli,Dkt. Asha Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ali wa Chama cha Mapinduzi CCM wameingia hatua ya tatu bora na kuwatupa nje Bernard Membe na Januari Makamba. Watatu hao sasa wameingia katika kikaango cha mwisho cha Mkutano Mkuu ambapo watapigiwa kura na hatimaye kumpata mmoja ambae atapeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, Aidha wamepigiwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa usiku huu na matokeo yanategemewa kutangazwa kesho Julai 12,2015 saa.4 asubuhi
Balozi Amina Salum Ali
Dk Asha Rose Migiro
Dk John Pombe Magufuli