Monthly Archives: November 2015

AGIZO LA RAIS

4509afe9-1ace-409f-81b4-f505070135f7

Sehemu  ambako utaanzia upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli la kutumia fedha shilingi bilioni  nne zilizopaswa kutumika kugharamia Shamrashamra za siku ya Uhuru Desemba 9, 2015 kutumika kufanya upanuzi wa barabara hiyo.

 

            TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.

Tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara hapa nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara moja

Akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika  barabara hiyo

Kujengwa kwa njia hizo kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano.

Wakati huo huo, Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo Prof. Lipumba amempongeza Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kwa kutoa hotuba nzuri ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokonga nyoyo za Watanzania.

Kwa Upande wake Rais Magufuli amempongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga ufisadi na amemtakia heri katika shughuli zake.

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.

Dar es Salaam.

 

30 Novemba,2015

 

 

 

RAIS MAGUFULI AONANA NA MABALOZI WA CHINA NA KOREA KUSINI PAMOJA NA PROFESA LIPUMBA IKULU NOVEMBA 30,2015

12fvvf vf

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015

1bfc9020-f6ae-42dc-bbe9-e7f9b8f9dcaa

 

 

83ec41a5-6dda-4b12-81c5-0eb83bbc9aa2

 

 

03e9346a-8d03-47a6-9be2-458933ce4032Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Korea ya Kusini  hapa nchini Mhe. Chung IL Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Balozi huyo pia alitumia nafasi hiyo kumuaga Rais kwa kuwa muda wake wa kufanya kazi nchini umemalizika.

6e00290a-8874-4100-afe6-ad1267f7e787

 

 

337b70ca-7868-4134-bf09-d1339aa45de0Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30,2015 Profesa Lipumba amempongeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma