Monthly Archives: December 2015

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ATANGAZA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU KATIBU WAKUU WAPYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM DESEMBA 30,2015

19dde182-bba4-4c41-ba9c-cbeecfad111f Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Ikulu jijini Dar es Salaam Desemba 30,2015. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakisikiliza kwa makini.    

ac3f9771-ce8d-40c7-8bc9-524a711bea1f

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwaonesha orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakishudia.

0e5b03dc-2932-47c9-b059-2a64d063cb75

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Mara baada ya kumkabidhi orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliwateua leo Ikulu jijini Dar es Salaam

ORODHA YA  MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU KATIBU WAKUU 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu katika Wizara mbalimbali.

Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

  1. Katibu Mkuu Kiongozi

Balozi – Ombeni Sefue

  1. Katibu Mkuu Ikulu

Peter Ilomo

  1. Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Dkt. Laurian Ndumbaro

  1. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)

Dkt. Deo  Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu – Afya)

Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu – Elimu)

  1. Ofisi ya Makamu wa Rais

Mbaraka A. Wakili ( Katibu Mkuu)

Mhandisi Ngosi Mwihava (Naibu Katibu Mkuu)

 

  1. Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)

Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira)

Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge)

Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu – Sera)

  1. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

Dkt. Frolence Turuka (Katibu Mkuu – Kilimo)

Dkt. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo)

Dkt. Budeba (Katibu Mkuu – Uvuvi)

 

  1. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Mhandisi Joseph. Nyamuhanga (Katibu Mkuu – Ujenzi)

Dkt. Leonard M. Chamuliho (Katibu Mkuu – Uchukuzi)

Profesa Faustine R. Kamuzora (Katibu Mkuu – Mawasiliano)

Mary Sassabo (Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano)

  1. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Dkt. Yamungu Kayandabira (Katibu Mkuu)

Dkt. Moses Kusiluka (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Maliasili na Utalii

Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu)

Anjelina Madete (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Dkt. Adelhem James Meru (Katibu Mkuu – Viwanda)

Profesa Adolf F. Mkenda (Katibu Mkuu – Biashara na Uwekezaji)

Mhandisi Joel Malongo (Naibu Katibu Mkuu)

 

  1. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

Maimuna Tarishi (Katibu Mkuu)

Profesa Simon S. Msanjila (Naibu Katibu Mkuu)

Dkt. Leonard Akwilapo (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katibu Mkuu – Afya)

Sihaba Nkinga (Katibu Mkuu – Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto)

  1.  Wizara ya Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo

Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel (Katibu Mkuu)

Nuru Halfan Mrisho (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Mhandisi Mbogo Futakamba (Katibu Mkuu)

Mhandisi Kalobero Emmanuel (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Nishati na Madini

Profesa Justus W. Ntalikwa (Katibu Mkuu)

Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu)

Dkt. Paulina Pallangyo (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Katiba na Sheria

Profesa Sifuni Mchome (Katibu Mkuu)

Suzan Paul Mlawi (Naibu Katibu Mkuu)

Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu)

  1.  Wizara ya Mambo ya Ndani

Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira (Katibu Mkuu)

Balozi Hassan Simba Yahaya (Naibu Katibu Mkuu)

 

  1.  Wizara ya Fedha na Mipango

Dkt. Silvacius Likwelile (Katibu Mkuu)

Dorothy Mwanyika (Naibu Katibu Mkuu)

James Dotto (Naibu Katibu Mkuu)

Amina Hamis Shaban (Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa

Dkt. Aziz Mlima (Katibu Mkuu)

Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi ( Naibu Katibu Mkuu)

  1. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Job D. Masima (Katibu Mkuu)

Immaculate Peter Ngwale (Naibu Katibu Mkuu

 

Makatibu wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao hawajatajwa katika orodha hii watapangiwa kazi nyingine.

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Eliakimu Maswi kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na ametengua uteuzi wa Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Lusekelo Mwaseba, ambaye atapangiwa kazi nyingine

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

30 Desemba, 2015