Daily Archives: April 15, 2016

RAIS WA SUDANI KUSINI SALVA KIIR AWASILI NCHINI NA KUTIA SAINI MKATABA WA NCHI YAKE KUJIUNGA RASMI NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI APRIL 15,2016

1 Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akipokea maua kutoka kwa mtoto Sharon Innocencia Shiyo mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli.

frrRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit ikulu jijini Dar es salaam alipowasili kwa ajili ya utiaji saini wa Mkataba wa Sudani Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki

2 Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki

3 Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu kwa ajili ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki

4Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

6 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kwenye mkataba wa kuiwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

7 Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akitia saini kwenye Mkataba wa Sudani Kusini kujiunga na Jumuia ya Afrika Mashariki.

8hhhhhh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akibadilishana makabrasha ya mkataba na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit mara baada ya kukamilika kwa zoezi la utiaji Saini wa kuiwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

40e56cc0-3265-46f6-8fc9-6b52fac1603eRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit wakiangalia kikundi cha ngoma Ikulu jijini Dar es salaam alipowasili kwa ajili ya utiaji saini wa Mkataba wa Sudani Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki

 

 

 

 

 

9 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit kabla ya utiaji saini wa Mkataba wa Sudani Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es Salaam April 15, 2016