Monthly Archives: March 2017

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA HAILEMARIAM DESSALEGN AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI MARCH 31,2017

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam March 31,2017

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn wakati nyimbo za mataifa mawili (Tanzania na Ethiopia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye jukwaa kwenda kukagua gwaride la Heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa kwa ajili yake

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn Ikulu jijini Dar es salaam

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akipiga ngoma mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpigia makofi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mkutano wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi kwa mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn Ikulu jijini Dar es Salaam.

Shamra shamra zikiendelea wakati wa kuwasili Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikaribishwa kwa kupewa ua na mtoto Xyleen Mapunda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam

 

 

 

 

 

 

 

 

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MHE. DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM MARCH 29,2017

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM jijini Dar es Salaam March 29,2017

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiwa pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Salim Ahmed Salim mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam