Daily Archives: October 8, 2018

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MTENDAJI WA SADC,BALOZI WA KENYA HAPA NCHINI PAMOJA NA KUPOKEA TAARIFA YA UJENZI WA OFISI YA MUDA YA IKULU YA CHAMWINO JIJINI DODOMA.OKTOBA 8,2018 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kikao cha kupokea Taarifa ya Maendeleo ya Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino Dodoma kutoka kwa wataalamu mbalimbali wanaohusika na ujenzi huo. Wakwanza kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Dkt. Moses Kusiluka

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam leo Oktoba 8, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stregomena L. Tax .Ikulu Jijini Dar es salaam.Oktoba 8, 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax wapili kutoka kushoto mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe wapili kutoka kulia akifatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara hiyo Bw. Shio. Kushoto ni Msaidizi wa Rais Maswala ya Diplomasia Balozi Zuhura Bundala

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Balozi wa Kenya nchini Mhe. Dkt. Dan Kazungu baada ya kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam. Oktoba 8, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Dkt. Dan Kazungu pamoja na Naibu Balozi wa Kenya Mhe. Boniface Muhia Ikulu jijini Dar es Salama

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa Hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 125 kutoka kwa Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Dkt. Dan Kazungu Kwa ajili ya Rambirambi ya nchi hiyo kwa Tanzania kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere huko Mwanza mwezi Septemba 20,2018

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katiia mazungumzo na Balozi wa Kenya hapa nchini  Mhe. Dkt. Dan Kazungu pamoja na Naibu Balozi wa Kenya Mhe. Boniface Muhia baada ya Balozi huyo kumkabidhi rais Magufuli jumla ya Shilingi milioni 125 za Rambirambi ya nchi hiyo kwa Tanzania kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere huko Mwanza mwezi uliopita. Hafla hii imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam.Oktoba 8, 2018