Daily Archives: November 16, 2018

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA KWA UKANDA WA AFRIKA HAFEZ GHANEM IKULU JIJINI DAR ES SALAAM-BENKI HIYO IMERIDHIA KUTOA DOLA MILIONI 300 KWA TANZANIA.NOVEMBA 16,2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Bella Bird Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem Ikulu jijini Dar es Salaam

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo yake na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem watatu kutoka kushoto Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird wapili kutoka kushoto akifatiwa na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird wapili kutoka kushoto akifatiwa na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga , Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu. Mstari wa nyuma wakwaza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Katibu Mku Wizara ya Fedha Doto James, Balozi Zuhuru Bundala pamoja na wageni wengine.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem Ikulu jijini Dar es Salaam aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem akizungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WAHUDHURIA MISA YA SHUKURANI YA UHAI YA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA KUTIMIZA UMRI WA MIAKA 80

Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimpa zawadi ya kadi na kisha kumpongeza Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa na mkewe Mama Anna Mkapa kwa kutimiza umri wa miaka 80 katika Misa ya Shukurani ya uhai iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam. Novemba 12, 2018

Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa pamoja na Maaskofu wakati wa Misa ya Shukrani kwa Mhe. Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam.Novemba 12, 2018

Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea kwa furaha na  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa baada ya  Misa ya Shukurani kwa  Mhe. Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata  jijini Dar es salaam.Novemba 12, 2018

Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Misa ya Shukurani ya  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam.Novemba 12, 2018.Kulia kwa Mhe. Mkapa ni mkewe Mama Anna Mkapa