Monthly Archives: May 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli awakabidhi Hati ya Makabidhiano ya zawadi ya Ndege aina ya Tausi 25 kwa marais wastaafu na Mama Maria Nyerere mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere hafla hiyo fupi ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.

.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika sherehe za  Makabidhiano ya zawadi ya Ndege aina ya Tausi 25 kwa  marais wastaafu na Mama Maria Nyerere mjane wa Baba wa Taifa  kwa ajili ya kuwafuga katika Makazi yake, hafla hiyo fupi ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Hati ya Makabidhiano ya zawadi ya Ndege aina ya Tausi 25 kwa Mama Maria Nyerere mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kuwafuga katika Makazi yake, hafla hiyo fupi ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Hati ya Makabidhiano ya zawadi ya Ndege aina ya Tausi 25 rais mstaafu Benjamin William Mkapa kwa ajili ya kuwafuga katika Makazi yake, hafla hiyo fupi ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ikulu, Chamwino.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Mei, 2020 amekagua maandalizi ya sherehe za uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma zitakazofanyika kesho tarehe 30 Mei, 2020.

Jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi hizo litawekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Maria Nyerere (kwa niaba ya Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere), Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi na zitarushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao.