Maafisa waandamizi wa Jeshi la Wananchi la Tanzania wakiwa
wamebeba Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Meja Jenerali mstaafu
Muhiddin Mfaume Kimario wakiwasili katika makaburi ya Manispaa ya
Moshi Mkoani Kilimanjaro Oktoba 11, 2014
: Rais kikwete akiwa na Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya (kushoto
kwa Rais) na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Ibrahim Msengi
(kulia) na Meja Jenerali Ezekiel Kyunga, mwakilishi wa Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange (kulia kwa Rais) wakati mwili wa
marehemu Meja Jenerali Mstaafu Muhiddin Mfaume Kimario ukiwasili
katika makaburi ya Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro Jumamosi
Oktoba 11, 2014
Waombolezaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu
Meja Jenerali mstaafu wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) Marehemu
Muhiddini Kimario katika makaburi ya manispaa ya Moshi mkoani
Kilimanjaro kwa mazishi Oktoka 11, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la
Meja Jenerali Mstaafu Muhiddin Mfaume Kimario wakati wa mazishi katika
makaburi ya Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro Oktoba 11,
2014
Rais Kikwete akimfariji mjane wa marehemu alipokwenda kutoa pole
baada ya mazishi
Rais Kikwete akiwafariji familia wa marehemu alipokwenda
kutoa pole baada ya mazishi