Daily Archives: April 25, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI DKT. LU YOUQING IKULU JIJINI DAR ES SALAAM APRIL 25,2016

111

 

222Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Dkt. Lu alifika Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumza masuala mbalimbali ya kimaendeleo na Rais Dkt. Magufuli.

3333Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing akimkabidhi Rais Dkt. John Pombe Magufuli ujumbe wa barua ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Rais wa China Xi Jinping Ikulu jijini Dar es Salaam

5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam

4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing wanne kutoka kushoto, Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa wapili kutoka kulia pamoja na maafisa wengine kutoka nchini na Ubalozi wa China.

 

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI LEO TAREHE 25 APRILI, 2016 AMEFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 25 YA TANZANIA BARA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Aprili, 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 25 ya Tanzania Bara. Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakisha katika vituo vyao vya sasa.  Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

 1. Arusha –                     Richard Kwitega
 2. Geita –                         Selestine Muhochi Gesimba
 3. Kagera –                      Armatus C. Msole
 4. Kilimanjaro –            Eng. Aisha Amour
 5. Pwani –                       Zuberi Mhina Samataba
 6. Shinyanga –                Albert Gabriel Msovela
 7. Singida –                     Dr. Angelina Mageni Lutambi
 8. Simiyu –                      Jumanne Abdallah Sagini
 9. Tabora –                     Dkt. Thea Medard Ntara
 10. Tanga –                       Eng. Zena Said

Makatibu Tawala waliobadilishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo;

 1. Kigoma –                     Charles Amos Pallangyo (Kutoka Mkoa wa Geita)
 2. Morogoro –                Dkt. John S. Ndunguru (Kutoka Mkoa wa Kigoma)

Makatibu Tawala waliobakishwa katika vituo vyao vya sasa vya kazi ni kama ifuatavyo;

 1. Dar es salaam –         Theresia Louis Mbando
 2. Dodoma –                  Rehema Hussein Madenge
 3. Iringa –                        Wamoja Ayubu Dickolagwa
 4. Katavi –                       CP Paul Chagonja
 5. Lindi –                         Ramadhan Habibu Kaswa
 6. Mara –                        Benedict Richard Ole Kuyan
 7. Manyara –                  Eliakimu Chacha Maswi
 8. Mbeya-                       Mariam Amri Mjunguja
 9. Mtwara –                     Alfred Cosmas Luanda
 10. Mwanza –                   CP. Clodwing Mathew Mtweve
 11. Njombe –                    Jackson Lesika Saitabau
 12. Rukwa –                      Symthies Emmanuel Pangisa
 13. Ruvuma –                    Hassan Mpali Bendeyeko

Makatibu Tawala wa Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, wataapishwa siku ya Jumatano tarehe 27 Aprili, 2016 saa tatu asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,

IKULU Dar es salaam

25 Aprili, 2016