Monthly Archives: July 2015

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA CHUO KIKUU CHA NEWCASTLE, AUSTRALIA JULAI 29, 2015

1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes na viongozi wa chuo kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.  

2WFREWER

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia  tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho. 

3

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes na viongozi wa chuo wakipata maelezo kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho. 

4 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.  

5 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viogozi wa chuo jukwaa kuu wakisimama wakati nyimbo za Taifa za Tanzania na Australia zikipigwa wakati wa kuanza kwa sherehe za kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho. 

6

 

7wasanii wa kabila la Wakakulang wakicheza ngoma za asili yao katika kunogesha sherehe za kihistorua ambapo Rais Kikwete amekuwa ni Mkuu wa Nchi wa kwanza kupokea digrii hiyo ya heshima kutoka katika Chuo hicho.

 

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA  SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA SHERIA (DOCTOR OF LAWS HONORIFIC CAUSA) NA CHUO KIKUU CHA NEWCASTLE .

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Chuo Kikuu cha Newcastle cha nchini Australia.

Sherehe za kumtunuku Rais shahada hiyo zimefanyika leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Newcastle.

Akisoma maelezo ya utangulizi katika hafla hiyo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans amesema Rais Kikwete ni Mkuu wa Nchi wa kwanza kupokea digrii hiyo ya heshima kutoka katika Chuo hicho.

Mkuu huyo wa Chuo amesema Rais Kikwete ametunukiwa shahada hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya duniani si kwa Tanzania tu bali  kwa Dunia nzima kwani mchango wake umetambulika  na  mashirika mbalimbali ya kimataifa yakiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Benki ya Dunia kwa ujumla.

“Tangu kuingia madarakani Rais Kikwete amechangia katika kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu , uchumi na Afya” amesema Bw. Jean na kuongeza kuwa “utawala wake umethibitishia sio Chuo cha Newcastle pekee bali pia kuonesha kanuni ya Msingi kuwa Elimu ni muhimu katika kukuza uchumi, uvumbuzi na katika maendeleo ya jamii” amesisitiza.

Tanzania imekua ikipokea misaada ya elimu kutoka Australia katika nyanja mbalimbali zikiwemo za madini, fedha, habari na tafiti mbalimbali ambazo zimeleta mabadiliko chanya katika jamii na duniani kwa ujumla.

Kwa sasa Watanzania wanne wanachukua masomo ya uzamifu katika masuala ya elimu na siasa.Tayari Watanzania 45 wamemaliza digrii na pia wapo watafiti kutoka Newcastle wanaofanya tafiti zao nchini Tanzania katika masuala ya elimu, afya na uhandisi.

Rais Kikwete ameshukuru na kuelezea jinsi alivyoguswa na tukio hilo ambapo ameushukuru uongozi wa Chuo hicho kwa kutambua mchango wake ambao ameelezea kuwa ameufanya wakati wa kipindi cha uongozi wake kwa moyo, upendo na nia njema kwa wananchi wote wa Tanzania na Dunia kwa ujumla.

“Ilikua nia yangu na wajibu wangu mkubwa kutumia ahadi nilizo waahidi wa Tanzania na hata zaidi ya kile nilicho ahidi na kuelezea kuwa mafanikio haya yote yamechangiwa pia kwa kiasi kikubwa na misingi imara iliyowekwa na viongozi walionitangulia upande wa Tanzania bara na Tanzania Visiwani kwa ujumla”

Katika utawala wake Rais Kikwete ametunukiwa shahada za heshima kutoka vyuo mbalimbali vya Marekani, Canada, China, Uturuki na Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam.

Rais Kikwete pia ametunukiwa tuzo za heshima mbalimbali katika masuala ya Kijamii (United Nations Social Good Award), Afya, Technolojia na Maendeleo (South-South Award for Global Health, Technology and Development) pamoja na Demokrasia (Icon of Democracy Award (Nertherlands)

Rais pia amepata kutunukiwa  na kutambuliwa kwa Mchango wake ambapo alitunukiwa nishani kadhaa zikiwemo;

1. (Most Excellent Order of the Peral of Africa) ambayo ni nishani ya juu nchini Uganda.

2. The order of the Green Crescent of the Comoros (Comoros)

3. Order of Abdulazizi Al Saud (Saudi Arabia)

4.Order of excellence (Jamaica)

5. Order of Oman (Oman)

6. AAI African National Achievement Award

7. U.S. Doctors for Africa Award

8. Good Governance in Africa  2015

Sherehe hiyo imehudhuriwa na Mstahiki Meya  wa mji wa Newcastle, Mama Nuatali Nelmes, walimu na wakufunzi wa Chuo cha Newcastle, wanafunzi wa Kitanzania na familia zao pamoja na Watanzania kadhaa wanaoishi na kufanya kazi katika mji wa Newcastle.

Rais Kikwete amekamilisha ziara yake ya Kiserikali ya siku nne nchini Australia na anatarajia kuelekea Dar-es Salaam tarehe 30 Julai, 2015

 

………..Mwisho……….

Imetolewa na:

Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi

Newcastle-Australia

29 Julai, 2015

 

RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA NA GAVANA MKUU WA NCHI HIYO 28 JULAI 2015

1

 

2wewwe Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015  katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney 

3Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015 katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney  

4Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la lililoandaliwa kwa heshima yake huku akipigiwa mizinga 21 alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai 2015 katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney

5Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiutambulisha ujumbe wake kwa Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe  28 Julai, 2015 katika makao  Makuu ya kiongozi  huyo  jijini Sydney 

6Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili kwenye jumba la serikali jijini Sydney tarehe 28 Julai 2015 na kukutana na kufanya mazungumzo na  Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove aliyesimama nyuma yake pamoja na Mama Salma Kikwete na Mke wa Gavana huyo Mama Cosgrove.  

7Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa chakula cha mchana kwenye jumba la serikali jijini Sydney tarehe 28 Julai 2015 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na  Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove.

 

 RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA JULAI 28,2015.

Waziri Mkuu wa Australia, Bwana Tony Abbot amempongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa  Katiba nchini Tanzania.

“Nakupongeza sana kwa uamuzi wako wa kukabidhi madaraka kwa amani nchini kwako , ni jambo la nadra sana Barani Afrika, kuwa na utaratibu mzuri na wa Amani  namna hii” Bw. Abbot amemuambia Rais Kikwete na kumueleza awe  na uhakika  kuwa ” Australia itaendelea kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kuleta maendeleo na kukuza  uchumi” ameongeza.

Rais Kikwete na Waziri Mkuu Abbot pia wamezungumzia jinsi nchi zao zinaweza kuendelea kushirikiana katika kulinda usalama baharini, kukuza zaidi ushirikiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii.

Rais Kikwete yuko nchini Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove.

Rais Kikwete amepokelewa leo asubuhi tarehe  28 katika makao  Makuu ya kiongozi  wa Australia kwa heshima zote kwa kupigiwa mizinga 21 na kuandaliwa chakula rasmi cha mchana na baadae kupanda mti  kuashiria kuimarisha mashirikiano baina ya nchi hizi mbili kwa kipindi kirefu kijacho.

Tanzania na Australia zimedumu katika ushirikiano  baina ya nchi zao tangu miaka ya sitini na sasa nchi mbili hizi zimeazimia kuimarisha mahusiano haya  zaidi katika sekta mbalimbali zikiwemo za uwekezaji na biashara kati yao.

Baadae leo jioni Rais Kikwete atakutana na wawekezaji wakubwa wa Australia ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania kwa ajili ya mazungumzo ya namna ya kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini na jinsi Tanzania inaweza kunufaika  kutokana na kupata gesi.

Tayari Serikali ya Australia na makampuni binafsi ya gesi na mafuta, yanaisaidia Tanzania hasa katika vyuo vya ufundi stadi VETA na  tafiti mbalimbali katika Kilimo.

Kesho tarehe 29 Julai, 2015 Rais Kikwete anatarajia kutunukiwa digrii ya udaktari wa heshima ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika uongozi kwa kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani nchini Tanzania na Dunia kwa ujumla.

Rais Kikwete anatarajia kuondoka Australia na kurejea Tanzania baada ya shughuli ya kupokea shahada yake na ratiba yake kwa ujumla.

Imetolewa na:

Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi

Canberra-Australia

28 Julai, 2015