Monthly Archives: February 2017

RAIS YOWERI MUSEVENI AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI TANZANIA NA KUREJEA NCHINI KWAKE FEBRUARI 26,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kwa ajili ya kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kabla ya kuondoka ma kurejea nchini kwake.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza kuelekea kwenye ndege mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za Mataifa mawili zilipokuwa zikipigwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakifurahia jambo wakati walipokwenda kumsindikiza Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla hajapanda ndege na kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.

Mmoja wa Mtumbuizaji Uwanjani hapo akionesha umahiri wake wa kupuliza Tarumbeta.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla hajapanda ndege na kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini

Benderea za Matifa mawili ya Uganda na Tanzania zikipepea Uwanjani hapo

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI PAMOJA NA MABALOZI WANNE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM FEBRUARI 26,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Thobias Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Februari 26,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Pindi Chana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Silima Kombo Haji kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sudani, Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (wapili kutoka kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba(Wakwanza kulia) , Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni (Wakwanza kushoto) pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye(Watatu kutoka kushoto waliosimama mstari wa nyuma) na Mabalozi Pindi Chana(Wakwanza kulia walisimama mstari wa nyuma ) , Balozi Matilda Masuka(Wapili kutoka kulia waliosimama mstari wa nyuma), Balozi Abdallah Kilima(Wapili kutoka kushoto mstari wa nyuma) na Balozi Silima Kombo Haji (Wakwanza kushoto waliosimama) mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Abdallah Kilima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Matilda Masuka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu pamoja na Mabalozi Pindi Chana, Balozi Silima Kombo Haji, Abdallah Kilima pamoja na Balozi Matilda Masuka mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.