Monthly Archives: March 2017

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI WA MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG), IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MARCH 27,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Nakala ya Vitabu vya Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam March 27,2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa anapiga makofi pamoja na Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupokea Ripoti hiyo kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hiyo Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Katibu Mkuu wa Ikulu Alphayo Kidata pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ripoti hiyo kutoka kwa CAG Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad akizungumza kabla ya kuwasilisha Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam

 

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hiyo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.

Maafisa kutoka katika Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakifatilia kwa makini wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HAFLA AMEPISHA MAWAZIRI, MABALOZI NA KAMISHNA WA MAHAKAMA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM MARCH 24,2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari wa vyombo mbalimbali baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na  waapishwa baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam Machi 24, 2017 Waapieshwa hao ni Mhe Jaji Stella Esther Mugasha ambaye ameapishwa kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Mhe Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Mhe Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Mhe. Dkt Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Mhe Profesa palamagamba Kabudi (Waziri wa sheria na katiba) na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, huku Waziri mpya wa Sheria na katiba Profesa palamagamba kabudi akiwa pembeni baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam  Machi 24, 2017

Waapishwa wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017. Kutoka kushoto ni Mhe Jaji Stella Esther Mugasha ambaye ameapishwa kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Mhe Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Mhe Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Mhe. Dkt Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Mhe Profesa palamagamba Kabudi (Waziri wa sheria na katiba) na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea machache  baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Profesa Palamagamba kabudi  baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Sheria na Katiba Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017