Monthly Archives: March 2018

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFUNGUA KIWANDA CHA SIGARA CHA MANSOOR INDUSTRIES LTD KILICHOPO KINGOLWIRA MOROGORO.MACHI 15,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda cha Sigara cha Mansoor Industries ltd kilichopo chini ya leseni ya Phillip Morris Tanzania katika eneo la Kingolwira mkoani Morogoro. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Phillip Morris Tanzania Dagmara Piasecka akipiga makofi, wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe pamoja na Mmiliki wa kiwanda cha Sigara Mansoor Shanif Hirani.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Tumbaku inayotumika katika utengenezaji wa Sigara hizo za Marlboro mara baada kufungua kiwanda hicho cha Sigara mkoani Morogoro.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mapakiti ya sigara hizo za Marlboro wakati akikagua utendaji kazi wa shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mara baada ya kukifungua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mojawapo ya hatua katika utengenezaji wa Sigara mara baada ya kufungua kiwanda hicho mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mojawapo ya vifungashio vya Sigara hizo kiwandani hapo mara baada ya kukifungua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Msanii mkongwe Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kuhutubia wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Msanii mkongwe Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kuimba katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Chifu Kingalu Mwanabanzi wa Kabila la Waluguru wa Morogoro mara baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi waliofika katika kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.

Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akipongezwa na baadhi ya wananchi mara baada ya kuimba wimbo wake wa Mimi ni Msanii katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe mara baada ya kuzindua kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.

 

Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa Mama Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro.

Mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa Mama Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro akichangiwa fedha na wadau mbalimbali mara baada ya kero yake kupatiwa ufumbuzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mmiliki wa kiwanda hicho cha Sigara Mansoor Shanif Hirani mara baada kufungua kiwanda hicho.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mzee Steven Mashishanga aliyewahi kuwa mkuu mkoa wa Morogoro mara baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi waliofika katika kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.Machi 15,2018.

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA SGR-KUTOKA MOROGORO HADI MAKUTUPORA- DODOMA KM 422 KATIKA ENEO LA IHUMWA NJE KIDOGO YA MJI WA DODOMA.MACHI 14,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke wakishuhudia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunga kifuniko mara baada ya kutumbukiza karatasi ya majina ya viongozi mbalimbali waliofanikisha ujenzi huo kama kumbukumbu katika uwekaji wa jiwe la msingi la Reli ya Kisasa(SGR) itakayotoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mfano wa Reli hiyo ya Kisasa mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mfano wa Reli hiyo ya Kisasa mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mfano wa Reli hiyo ya Kisasa mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wabunge waliofika kwenye uzinduzi wa Reli hiyo ya Kisasa SGR itakayo toka Morogoro hadi Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Reli hio ya Kisasa katika eneo la Ihumwa Stesheni mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru madereva wa magari yatakayofanya kazi ya ujenzi wa reli hiyo ya kisasa SGR itakayo toka Morogoro hadi Dodoma.

Sehemu ya wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi.

Treni ya zamani ikipita katika Reli za zamani katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili katika eneo la Ihumwa Stesheni kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi.

Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa akitoa maelezo ya mradi huo wa Reli ya kisasa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.